Amani! Cuk Yashiriki Katika Kampeni ZA Kueneza Ujumbe WA Amani Nchini Kenya

Hayawi Hayawi huwa! Siku ya kujua mbivu na mbichi katika maswala ya uongozi wa nchi ya Kenya imekaribia. Hivyo basi, tarehe 22,7/2022 baraza la kutawala la  wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika, (CUK) iliandaa kampeni  za amani ili kueneza ujumbe maalum wa umuhimu wa amani kabla na baada ya uchaguzi mkuu kufanyika.

Rais wa baraza la wanafunzi wa CUK Bw. Collins pamoja na wanafunzi wenzake katika sherehe ya siku ya Amani chuoni CUK

Hafla hii, ilikusudia  kuwaelimisha wanafunzi, wakufunzi, pamwe na wafanyikazi mbalimbali wa CUK,  umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi mkuu, kufanya kampeni mbalimbali kwa amani, kuchagua viongozi wetu bila vita na punde tu, majibu yanapotangazwa,adinasi wote  wakubali matokeo ya uchaguzi mkuu na kuendelea na masomo, kazi na shughuli mbalimbali. Vilevile, kampeni hii ilikuwa na lengo ya kuwatahadharisha vijana kutokana na uzoevu wa kutumiwa kama ajenti  vita na vurugu.

Prof. Esther Gicheru, naibu makamu chansela wa mipango na utawala wa fedha wa chuo kikuu cha CUK awahotubia waalikwa kuhusu umihimu wa kudumisha amani

Waliohudhuria kampeni hii na kuwapa wanafunzi wa CUK na wote waliohudhuria,  wosia mufti ni baadhi ya viongozi wa chuo kikuu cha CUK, ikiwemo, Profesa Esther Gicheru ambaye ni naibu makamu chansela wa mipango na utawala wa fedha, Dkt. Lucinda Mugaa,  mkuu wa wanafunzi katika chuo kikuu cha CUK, viongozi mbalimbali wa Mkenya Daima– shikrika la kueneza ujumbe wa amani, viongozi mbalimbali wa maswala ya vijana, sikwambi, mabaraza ya wanafunzi ya vyuo mbalimbali mjini Nairobi.

 

Kilichosisitizwa zaidi katika hafla hii ni umuhimu wa Amani. Ama kwa hakika,baraza la kutawala la  wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika,  pamoja na waliohudhuria waliweza kutimiza lengo na  wajibu wao wa kuwaelimisha wanajamii wa maeneo ya Karen na Gataka kuhusu umuhimu wa kudumisha amani msimu huu wa uchaguzi.

Wengi walisisitiza maneno ya mababu wetu wa kale na kusadiki kuwa watapiga kura na kupokea majibu kwa kwani wanaelewa fika kuwa, asiyekubali kushindwa, si mshindani.

Kaditama, udugu wote wa CUK ungependa kukuomba ewe somaji mpendwa,  kueneza ujumbe wa amani na kuimba wimbo wa umoja haswa wakati huu wa uchaguzi na hata baada ya uchaguzi mkuu ili sote tuweze kuwa na uchaguzi wenye amani na umoja.

Aisee! Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.

#tusibleed ndio walead#.

kwaya barabara ya CUK yawatumbuiza waalikwa kwa nyimbo nzuri za kueneza amani

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Find us on social media

University bank accounts

All payments to the institution are payable to the Co-operative Bank of Kenya and Equity Bank Kenya
Co-operative Bank –Account No.01129062663600 (Karen Branch). The University does not accept cash payments
Equity Bank of Kenya-Account Number 1250277107862(Karen Supreme branch)

Mpesa payment option

Procedure for fee payment through M-Pesa:

  1. Go to M-Pesa;
  2. Select pay bill or pay with M-Pesa then pay bill;
  3. Enter business number 728176;
  4. Enter account number (e.g BCMC01/0001/2022);
  5. Enter amount;
  6. Enter your M-Pesa PIN;
  7. Confirm the details then press OK.

N/B: You’ll get 2 messages, 1 from M-Pesa and the other from cooperative bank of Kenya showing that your payment has gone through.

Scroll to Top