Amani! Cuk Yashiriki Katika Kampeni ZA Kueneza Ujumbe WA Amani Nchini Kenya
Hayawi Hayawi huwa! Siku ya kujua mbivu na mbichi katika maswala ya uongozi wa nchi ya Kenya imekaribia. Hivyo basi, tarehe 22,7/2022 baraza la kutawala la wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika, (CUK) iliandaa kampeni za amani ili kueneza ujumbe maalum wa umuhimu wa amani kabla na baada ya uchaguzi mkuu kufanyika. Rais wa baraza la wanafunzi wa CUK Bw. Collins pamoja na wanafunzi wenzake katika sherehe ya siku ya Amani chuoni CUK Hafla hii, ilikusudia kuwaelimisha wanafunzi, wakufunzi, pamwe na wafanyikazi mbalimbali wa CUK, umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi mkuu, kufanya kampeni mbalimbali kwa amani, kuchagua viongozi wetu bila vita na punde tu, majibu yanapotangazwa,adinasi wote wakubali matokeo ya uchaguzi mkuu na kuendelea na masomo, kazi na shughuli mbalimbali. Vilevile, kampeni hii ilikuwa na lengo ya kuwatahadharisha vijana kutokana na uzoevu wa kutumiwa kama ajenti vita na vurugu. Prof. Esther Gicheru, naibu makamu chansela wa mipango na utawala wa fedha wa chuo kikuu cha CUK awahotubia waalikwa kuhusu umihimu wa kudumisha amani Waliohudhuria kampeni hii na kuwapa wanafunzi wa CUK na wote waliohudhuria, wosia mufti ni baadhi ya viongozi wa chuo kikuu cha CUK, ikiwemo, Profesa Esther Gicheru ambaye ni naibu makamu chansela wa mipango na utawala wa fedha, Dkt. Lucinda Mugaa, mkuu wa wanafunzi katika chuo kikuu cha CUK, viongozi mbalimbali wa Mkenya Daima– shikrika la kueneza ujumbe wa amani, viongozi mbalimbali wa maswala ya vijana, sikwambi, mabaraza ya wanafunzi ya vyuo mbalimbali mjini Nairobi. Kilichosisitizwa zaidi katika hafla hii ni umuhimu wa Amani. Ama kwa hakika,baraza la kutawala la wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika, pamoja na waliohudhuria waliweza kutimiza lengo na wajibu wao wa kuwaelimisha wanajamii wa maeneo ya Karen na Gataka kuhusu umuhimu wa kudumisha amani msimu huu wa uchaguzi. Wengi walisisitiza maneno ya mababu wetu wa kale na kusadiki kuwa watapiga kura na kupokea majibu kwa kwani wanaelewa fika kuwa, asiyekubali kushindwa, si mshindani. Kaditama, udugu wote wa CUK ungependa kukuomba ewe somaji mpendwa, kueneza ujumbe wa amani na kuimba wimbo wa umoja haswa wakati huu wa uchaguzi na hata baada ya uchaguzi mkuu ili sote tuweze kuwa na uchaguzi wenye amani na umoja. Aisee! Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. #tusibleed ndio walead#. kwaya barabara ya CUK yawatumbuiza waalikwa kwa nyimbo nzuri za kueneza amani
Amani! Cuk Yashiriki Katika Kampeni ZA Kueneza Ujumbe WA Amani Nchini Kenya Read More »